Mshambuliaji wa Yanga raia wa Liberia Kpah Sherman anaondoka leo (Jumatatu) kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na kama atafuzu vipimo hivyo, moja kwa moja atajiunga na klabu ya Black Aces ambayo inashiriki ligi kuu ya nchini Afrika Kusini.
Katibu mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema, Sherman anaondoka leo jioni kuelekea Afrika Kusini kufanyiwa vipimo na kama atafuzu basi atasaini mkatba na klabu itapata chake na yeye (Sherman) atapata haki yake.
“Ni utaratibu tu, ambapo mchezaji anapotakiwa na timu ni lazima aitwe ili kukamilisha taratibu za vipimo vya afya then baada ya hapo atasaini, klabu itapata chake na yeye atapata chake na ataendelea na utaratibu mwingine wa kucheza soka nafikiri ataondoka leo jioni”, amesema Tiboroha.
Sherman amekuwa hana namba ya kudumu kwenye kikosi cha Yanga kutona na mwalimu Hans van Pluijm kumtumia Amis Tambwe kama mshambuliaji namba moja kwenye kikosi cha wanajangwani, kusajiliwa kwa washambuliaji wapya Donald Ngoma na Malimi Busungu kwenye kikosi cha Yanga, kumezidi kupoteza matumaini ya mliberia huyo kupata nafasi kwenye kiosi cha kwanza cha klabu hiyo.

No comments:
Post a Comment