Katika hali isiyokuwa ya kawaida, barua aliyoandika kocha wa zamani wa Liverpool, mwenye historia kubwa, BILL SHANKLY akiomba kustaafu mwaka 1974 imeonekana.
Akiaminika kuwa ndiye kocha mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika soka la England, Shankly aliyefariki dunia mwaka 1981 akiwa na miaka 68 aliifundisha Liverpool kwa mafanikio katika kipindi cha miaka 15 kabla ya kustaafu.
Nyaraka hiyo imefichuliwa na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, JOHN ALDRIDGE katika maktaba ya HOTELI YA SHANKLY na baada ya hapo akaandika kwenye mtandao wake wa Twitter akisema hii ndio barua aliyoandika akiomba kustaafu.
Barua hiyo aliyoandika Juni 18, 1974 iliwasilishwa kwa mwenyekiti wa Liverpool wa wakati huo, JOHN SMITH akisomeka kwamba , SHANKLY anaomba kustaafu kuifundisha Liverpool haraka iwezekanavyo na litakuwa jambo zuri kama klabu hiyo itaanza kuandaa mafao yake.
Maombi hayo yalikubaliwa na Smith Julai 12 mwaka huo ambapo aliitisha mkutano na waandishi wa habari akisema kuwa Liverpool imepokea maombi ya ya kujiuzulu kwa kocha wao na bodi ya klabu imekubali, huku akimshukuru kwa mchango mkubwa aliotoa Anfield.
Chanzo:shafii dauda
No comments:
Post a Comment