.

.

TUMIA VIDOLE

TUMIA VIDOLE
PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918 PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918sundwa.Blogspot.com

Monday, July 27, 2015

HATIMAYE KEVIN DE BRUYNE ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA

Kinda wa zamani wa klabu ya Chelsea raia wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne
hatimaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka nchini Ujerumani na
kuwabwaga wachezaji wawili wa Bayern Munich, Arjen Robben na Manuel
Nueur ambao ndo walikuwa wapinzani wake kwenye kinyang’anyiro hicho.

De Bruyne alipata kura 367 huku Robben akipata kura 94 na Neuer
akipata kura 67. Kumbuka msimu uliopita Mbelgiji huyu alifunga magoli
10 huku akitoa assist 20, bila shaka huu ulikuwa msimu mzuri sana kwa
kijana huyu ambaye kwa sasa anahusishwa kuhamia pale Etihad…
Kutokana na kutopata nafasi katika klabu yake ya zamani ya chelsea, De
Bruyne alienda Wolfsburg ambapo ameiwezesha timu hii kumaliza nyuma ya
bingwa Bayern Munich huku akiisaidia timu yake kutwaa kombe la
DFB-Pokal.

Pia kocha wa Wolfsburg Dieter Hecking alitajwa kama kocha bora wa
msimu baada ya kukusanya kura 203. Makocha wengine kama Markus
Weinzierl wa Augsburg, Lucien Favre, Jurgen Klopp na Pep Gurdiola
walimaliza nyuma.
kevin-de-bruyne-wolfsburg-europa-league_1bne4fkc02vsn1ppf88zb1ouzh

No comments:

Post a Comment