Mugiraneza 03
Katika harakati za kuhakikisha inakiimarisha kikosi chake kwa ajili ya ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuanza hivi karibuni pamoja na michuano ya kimataifa, klabu ya Azam FC imemsajili mchezaji wa kimataifa Jean-Buptiste Mugiraneza ‘Migi’ ambaye ni kiungo wa kimataifa wa Ruanda lakini nyota huyo hataitumikia Azam katika michuano ya Kagame.
“Tumeweza kufanya mazungumzo na mchezaji Mugiraneza, alikuja hapa wakati tunaelekea Tanga na alibahatika kucheza mechi zote mbili kwahiyo mwalimu alikuwa anasikia sifa zake, amemuona na amethibitisha kuwa anaweza kuwa mmoja kati ya wachezaji wake wa Azam”, amesema Jafar Idd, afisa habari wa Azam FC.
Mugiraneza 02
“Ameingia mkataba wa miaka miwili na Azam leo mchana kwa makubaliano kwamba kwenye michuano ya Kagame atacheza kwenye timu yake ya APR lakini baada ya Kagame atakuwa ameingia rasmi kwenye klabu ya Azam FC na kikubwa ni kwamba uwezo wa mchezajin huyo unajulikana kwa wapenda soka wote kwamba Mugiraneza ni mchezaji wa aina gani na ameshacheza kwenye mashindano mbali mbali”, ameongeza.
“Kwahiyo mwalimu alimuona mwaka jana kwenye michuano kama hii ya Kagame, mwaka huu tena amemfuatilia na kuona kipaji chake na uwezo wake alionao kwenye timu, atatoa mchango mkubwa sana kwa Azam, kwahiyo leo amesaini rasmi na baada ya Kagame ataungana na timu kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara”, aliendelea kufafanua.
Mugiraneza 01
“Huyu mchezaji atakuwa ni wa tatu kumsajili msimu huu, tulimsajili Ame Ally maarufu kama Zungu kutoka Mtibwa, tumesajili mchezaji huru wa kitanzania Ramadhani Singano ‘Messi’ na leo tena tumesajili mchezaji mwingine wa kimataifa Mugiraneza ambaye tayari amecheza mechi mbili za kirafiki akiwa Azam”, alimaliza.
No comments:
Post a Comment