Uongozi wa Mbeya City umewatoa hofu mashabiki wao kuhusu suala la usajili wa wachezaji watakao kiumikia kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao kwa kusema benchi la ufundi limefanya uchaguzi sahihi wa nyota wapya watakaowasajili.
Katibu mkuu wa Mbeya City Emanuel Kimbe amesisitiza pia kuwa mfumo utakaotumika hauna tofauti na ule walioutumia msimu uliopita.
“Mfumo ni uleule na wategemee kuona sura nyingine mpya kabisa ambazo hawajawahi kuziona wala kuzisikia, kwasababu nakumbuka mzunguko wa pili wa msimu uliopita walimuona mtu kama Rafael ambaye walikuwa hawamjui na wakaona kuwa alikuwa ni kiungo bora kabisa”, amesema Kimbe.
“Kwahiyo wategemee kuona chipukizi wengine wakija kuchukua nafasi wakiwa na viwango vya juu kabisa, Mbeya City iliyomaliza ligi msimu uliomalizika imeondokewa na wachezaji watatu tu, lakini timu kubwa bado ipo. Wachezaji watatu walioondoka kati ya 11 bado tunaamini wachezaji waliopo bado watafanya vizuri”, ameongeza.
Mbeya City imeshaondokewa na wachezaji wasiopungua watano ambao walikuwa kwenye kikosi cha kwanza lakini mpaka sasahivi bado hawajamtangaza hata hata mchezaji mmoja waliyemsajili kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao unaotarajiwa kuanza katikati ya mwezi Agosti mwaka huu.
No comments:
Post a Comment