.

.

TUMIA VIDOLE

TUMIA VIDOLE
PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918 PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918sundwa.Blogspot.com

Wednesday, July 15, 2015

ACHA KABISA : Waliwahi kudharauliwa, wakaibuka mashujaa baadaye

MICHEZO:

SIO mastaa wote ambao walianza maisha yao ya soka kiulaini. Wapo ambao waliwahi kudharauliwa, wakaonekana nyanya, lakini baadaye waliibuka kuwa roho katika timu zao au timu nyingine. Hawa ni baadhi.

David de Gea

Kipa huyu Mhispaniola aliigharimu Manchester United dau la Pauni 18 milioni Juni 2011 na kuwa kipa ghali England. Katika pambano lake la kwanza tu la ngao ya jamii dhidi ya Man City aliruhusu mabao ya kizembe. Baadaye alijulikana kwa makosa ya kijinga uwanjani. Baadaye aliachana na ujinga huu na kwa sasa amepandisha kiwango chake huku akitajwa kuwa mmoja kati ya makipa watatu bora duniani.

Gareth Bale

Ni vigumu kuamini kuwa mchezaji huyu ghali zaidi duniani kuna wakati alikuwa kichekesho tu. Mwaka 2009 ilikuwa ngumu kuamini kuwa Gareth Bale siku moja angekuwa mchezaji ghali duniani. Staa huyu wa Wales kuna wakati aliwahi kuambiwa ana nuksi baada ya Tottenham kushindwa kushinda mechi yoyote ile katika mechi 24 za kwanza ambazo Bale aliichezea timu hyo. Januari 2010 ilidaiwa kuwa Birmingham City walikuwa wanaandaa dau la Pauni 3 milioni kwa ajili ya kumchukua staa huyo aliyechemka Tottenham. Ghafla maisha yakaanza kumnyookea Bale. Kilichobaki hadi sasa ni historia.

Aaron Ramsey

Maisha ya soka ya Aaron Ramsey Arsenal yalipata balaa pale alipovunjwa mguu na mlinzi wa Stoke City, Ryan Showcross Februari 2010 katika dimba la Brittania. Aliporudi uwanjani kujiamini kwake kulipotea na fomu yake ikaondoka. Alipelekwa kwa mikopo katika klabu za Nottingham Forest na Cardiff. Baadaye kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alikiri kwamba alikuwa anataka kutompanga mechi za Uwanja wa Emirates kwa sababu alikuwa anazomewa sana na mashabiki. Hata hivyo, msimu wa 2013/14, Ramsey alibadiika ghafla na kufunga mabao 10 katika mechi 23 za ligi. Alifunga bao murua pia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa sasa ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo Arsenal.

Cristiano Ronaldo

Wakati Cristiano Ronaldo alipohamia Manchester United kwa mara ya kwanza akitokea Sporting Lisbon mwaka 2003, kulikuwa na wasiwasi kuhusu kipaji chake. Alikosolewa sana kwa kuonekana anafanya kazi bure uwanjani. Alikuwa akipiga chenga nyingi bila ya kuzalisha chochote. Hata hivyo ghafla alibadilika na kuwa mchezaji hatari uwanjani kwa kufunga mabao mengi na kupika mabao lukuki

Jordan Henderson

Haikuchukua muda mrefu baada ya Liverpool kutoa Pauni 20 milioni kwa Sunderland kumchukua Jordan Henderson uhamisho huo ulikosolewa vikali. Mashabiki hawakuamini kama kijana huyu alikuwa mzuri vya kutosha. Mkurugenzi wa ufundi wa zamani wa Liverpool, Damien Comolli inadaiwa kuwa alifukuzwa kazi hiyo kwa sababu ya kumnunua Henderson. Hata hivyo, katika msimu wake wa tatu Liverpool, Henderson aliibuka kuwa mchezaji tegemeo Liverpool. Kwa sasa amepewa unahodha kabisa ambao umeachwa wazi na Steven Gerard aliyekwenda Marekani.

No comments:

Post a Comment