![]() |
Jengo la kituo cha Polisi likiteketea kwa moto |
Alisema kabla ya kuchomwa kituo hicho dereva aliyetambulika kwa jina la Yohana John aliyekuwa akiendesha gari aina ya Coaster alisababisha ajali katika eneo hilo na kumgonga mwanafunzi mmoja wa shule ya Bunjua ‘A’ Radhia Omary na kusababisha kifo chake.
Alisema baada ya mwanafunzi huyo kupoteza maisha wanafunzi wa shule hiyo pamoja na wananchi wa eneo hilo walikusanyika na kulala barabarani hali iliyosababaisha magari kutoendelea na safari zake.
Alisema wananchi hao pamoja na wanafunzi walifunga barabara hiyo kwa muda wa saa tatu wakidai kuwa wanataka matuta yawekwe katika eneo hilo lililopo karibu na shule hiyo ili liweze kuwasaidia wanafunzi wakati wa kuvuka barabara.
Hali hiyo ilileta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo kwa kufungwa na kushindwa kuendelea na shughuli zao hali iliyosababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya watu.
“Baada ya tukio hilo polisi na Tanroads tulikaa kikao cha dharura kilichokuwa kikielekeza utengenezwaji wa matuta ya haraka katika eneo hilo.
“Wakati tukiendelea na mazungumzo hayo wananchi walipata mwanya wa kukivamia kituo hicho na kukichoma moto.
“Sababu ya wananchi hao kuchoma kituo hicho hakuna, na wamefanya jambo ambalo si la busara na wamesahau kuwa kituo hicho kinawasaidia watu wote wa eneo hilo,”
alisema Kamanda Wambura. Alisema mbali na kuchoma kituo hicho pia wamechoma magari mamne ya watu binafsi yaliyokuwa yameegeshwa pembezoni mwa kituo hicho.
Pia alisema wanamshikilia dereva wa Coaster aliyesababisha ajali pamoja na gari hilo.
alisema Kamanda Wambura. Shuhuda wa tukio hilo, Moshi Sultan, alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 3:00 asubuhi baada ya gari kumgonga mwanafunzi huyo aliyekuwa anakwenda shule.Pia alisema wanamshikilia dereva wa Coaster aliyesababisha ajali pamoja na gari hilo.
“Kwa sasa tupo katika zoezi la kuwasaka na kuwakamata watu wote waliosababisha vurugu hizo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,”
Alisema baada ya tukio hilo wananchi wa eneo hilo walikusanyika na kufunga barabara hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na kuanza mvutano kati yao na hatimaye wananchi hao kuvamia kituo hicho na kukichoma moto.
No comments:
Post a Comment