BUTIHAMA MARA:
Wananchi wa wilaya ya Butiama Mkoani Mara wanakabiliwa na njaa kali hivyo wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka za kupeleka chakula cha msaada katika kunusuru maisha ya watu ambayo sasa imesababisha baadhi ya familia kuishi kwa kunywa uji.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ambao umeitishwa na mbunge wa jimbo hilo la Musoma Vijijini,wananchi wa kata ya Mugango na vijiji jirani katika wilaya ya butiama,wamesema eneo hilo hivi sasa linakabiliwa na njaa kali hivyo kunahitaji msaada wa haraka wa chakula ili kuokoa maisha ya wananchi.
Hata hivyo mbunge wa jimbo la Musoma vijiji Mh. Nimrod Mkono,amekiri wilaya hiyo kukabiliwa na njaa kali na kusema tayari amewasiliana na ofisi ya waziri Mkuu kwa ajili ya kuona namna ya kutoa msaada wa haraka wa chakula katika kukabiliana na njaa hiyo.
Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa mara Kapt.Mstaafu Asseri Msangi kwa nyakati tofauti amemweeleza waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda na makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal kuwa mkoa wa mara unakabiliwa na njaa kali,ambayo amesema imetoka na ukame pamoja na zao la muhogo kushambuliwa na ugonjwa wa batoto kali hivyo kuhitaji haraka tani zaidi ya elfu kumi za
chakula.
No comments:
Post a Comment