.

.

TUMIA VIDOLE

TUMIA VIDOLE
PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918 PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918sundwa.Blogspot.com

Tuesday, July 14, 2015

MICHEZO:


pichani ni kipa wa simba Ivo mapunda

Makipa wa Klabu ya Simba, Ivo Mapunda na yosso Peter Manyika 'Jr', wamekalia kuti kavu baada ya Kocha wa Makipa Mkenya, Abdul Salim, kutoridhika na uwezo wa makipa hao ambao waliidakia timu hiyo katika msimu wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliomalizika, imefahamika.

Mbali na makipa hao waliodaka msimu uliopita ambao wako kambini Lushoto, Tanga, pia wapo yosso wawili kutoka timu ya vijana ya umri chini ya miaka 20 (Simba B) akiwamo Denis Richard.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa viongozi wa juu wa Simba, alisema kocha huyo wa makipa amewaangalia wachezaji hao na kutoa taarifa ya awali kwa uongozi kwamba kuna haja ya kusajiliwa kipa mzoefu ambaye ataisaidia timu kufikia malengo yake. Kiongozi huyo alisema Mapunda mbali na kuwa mzoefu, kwa sasa amekuwa ni mchezaji ambaye anapata majeruhi mara kwa mara hivyo kumsababishia kukaa nje ya kikosi.

Alisema, pia kocha huyo wa makipa ambaye alimfundisha Mapunda katika timu ya Gor Mahia ya Kenya, alimuelezea mlinda mlango huyo wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Yanga, Prisons na St. George ya Ethiopia kwamba ni mahiri zaidi kwenye penalti kuliko kuwahi mashambulizi mengine ambayo ndiyo hupigwa mara kwa mara kwenye mechi.

Kiongozi huyo mwenye nguvu ndani ya Simba, aliongeza kuwa: "Kocha amesema Manyika anatakiwa kupewa mafunzo zaidi ya kuboresha kipaji chake wakati Dennis ambaye amemuona ni mbadala wa Mapunda, anahitaji miaka miwili ili kupata uzoefu wa kudaka kwenye ligi hiyo.

"Amesema hatuna kipa, Mapunda hayuko katika ubora wake, Manyika naye hayuko makini na ana mizaha isiyotakiwa kwa nafasi yake na Dennis anahitaki kupata muda zaidi kunolewa, ila atakuwa tishio na ana vitu adimu."
Kipa mwingine wa timu hiyo ni Hussein Shariff 'Cassilas' ambaye mwaka jana alikuwa majeruhi kwa muda mrefu na sasa hayuko Lushoto.

Taarifa za awali zinasema kuwa Cassilas anatarajiwa kurejea katika timu yake ya Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro kwa mkopo kwa sababu mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi umebakiza mwaka mmoja.
Rais wa Simba, Evans Aveva, alikataa kuzungumzia ripoti hiyo ya kocha wa makipa na kusema kwamba bado klabu yake inaendelea na zoezi la usajili kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi.

Simba inahitaji kujiimarisha kila idara ili iweze kufanya vizuri katika msimu ujao baada ya kumaliza kwenye nafasi ya tatu msimu uliopita na kukosa nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa hapo mwakani.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment