.

.

TUMIA VIDOLE

TUMIA VIDOLE
PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918 PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918sundwa.Blogspot.com

Tuesday, July 14, 2015

MALENGO: Kerr aota ubingwa Simba


kocha wa simba Kerry

Lushoto. Kocha wa Simba, Dylan Kerr amesema anakiandaa kikosi chake  kuhakikisha anatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/16.

Kerr alianza kazi ya kuifundisha Simba mapema mwezi huu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili mwishoni mwa Juni akipokea mikoba ya Mserbia, Goran Kopunovic aliyetimka mwishoni mwa msimu uliopita.

Simba haijachukua ubingwa tangu msimu wa 2011-12, tangu wakati huo imeshindwa kumaliza katika nafasi mbili za juu na kucheza mashindano ya kimataifa jambo linalowaumiza mashabiki wa timu hiyo.

Kocha huyo raia wa Uingereza alisema anatambua mabosi wake wanatamani timu imalize katika nafasi hizo mbili za juu hivyo ni lazima wachezaji wake wafanye kazi ya ziada katika hilo kwani Simba ni timu kubwa na ina kila sababu ya kumaliza katika nafasi hizo mbili.

“Nafasi mbili za juu ndiyo muhimu kwetu, ni kazi ambayo inabidi ifanyike, mimi kama kocha natakiwa kuifanya, pia wachezaji nao wanatakiwa kuifanya kazi hiyo.

“Wachezaji wanatakiwa kuamua wanataka kuiona timu yao inarudisha heshima, hapo tutakwenda sambamba,” alisema Kerr.

“Msimu ujao timu inatakiwa iwe na tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa, hayo ndiyo malengo yangu kama kocha, napenda kuwa na timu inayoshiriki michuano mikubwa.”

Simba imezikosa nafasi mbili za juu kwa misimu mitatu mfululizo kutokana na uimara wa Yanga na Azam ambazo zimekuwa zikibadilishana nafasi hizo.

Wakati huohuo, Simba iliendelea na mazoezi yake jana asubuhi mjini hapa na wachezaji walifanyishwa mazoezi ya kutengeneza kasi pamoja na  ufundi kidogo.

Awali, kocha Kerr alitoa mapumziko kwa wachezaji wake wote kuanzia Jumamosi mchana na kuwapa uhuru wa kutembea mjini hapa, lakini walitakiwa wote kuwa hotelini majira ya saa 12 jioni.

“Leo tunafanya mazoezi ya kasi uwanjani pamoja na ufundi kidogo katika mpira, nafurahi kikosi kinaendelea kuimarika na baada ya wiki hii nadhani tutakuwa katika kiwango kizuri zaidi,” alisema Kerr.

Kwa upande mwingine nyota wa timu hiyo ambao walikuwa na timu ya Taifa Stars tayari wamejiunga na wenzao hapa Lushoto, lakini wawili kati yao ni majeruhi na wanaweza wasifanye mazoezi yoyote.

No comments:

Post a Comment