Msanii Juma Kassim Nature almaarufu kama kiroboto amefunguka na kusema kuwa haoni sababu ya yeye kukimbizana au kuwa na papara katika mambo yake kwani yeye anaamini kuwa papara huwa na madhara yake katika kila jambo.
Nature alisema hayo kupitia mitandao ya kijamii na kusisitiza kuwa haoni sababu ya yeye kushindana na watu wengine kwani anaamini kuwa yeye kama kuweza anaweza na alishaweza toka kitambo hivyo haoni sababu ya kuwadondosha wenzake.
Kauli ya Juma Nature imepokewa kwa namna mbalimbali na mashabiki wake huku wengine wakisema mkali huyo alikuwa anafikisha ujumbe kwa wasanii wa sasa wa bongo fleva ambao wanaonekana kwenda na kasi na mabadiliko na muziki huku wengine wakionesha wazi kuwa wanashindana au kuoneshana katika tasnia hiyo.
Kufuatia hali hiyo ya mashindano ya mabadiliko ya hali ya juu mkali huyo ndipo aliposema kuwa ni bora aonekane mjinga kuliko kuwa na mbio za sakafuni kwa kuwa anaamini yeye hashindani na mtu ila anafanya kazi zake mwenyewe.
"Sinaga papara kabisaa speed yangu ado ado, bora kuitwa mjinga kuliko mbio za sakafuni sishindani na mtu kama kujua najua kitambo ni wadondoshe wenzangu kisa nini?
Alihoji." Juma Nature Kauli hii inathibitisha kuwa Juma Nature hawezi kufanya maamuzi au kubadilika kwa sababu tu kuna watu wamebadilika au wanafanya jambo fulani ila anaonesha wazi kuwa anafanya jambo vile ambavyo yeye amepanga na vile ambavyo yeye anaamini ndivyo inatakiwa kufanywa.
Baaada ya kuweka ujumbe huo katika mitandao yake ya kijamii moja ya shabiki wa Juma Nature alionesha kuelewa ujumbe huo ambao aliufikisha kisanaa baada ya kuweka picha ya Speed Meter ya gari huku ikionesha kuwa speed sifuri ili hali gari ikionekana kuwa kwenye mwendo.
"tumekuelewa mkubwa hapo umezungumzia mambo mengi sana hususani mziki wako" mbali na shabiki huyo lakini shabiki mwingine aliyefahamika kwa jina la Adolph Yamsebo alikuwa na haya juu ya mkali huyo ambaye alitamba na ngoma kibao enzi za nyuma katika tasnia ya bongo fleva.
"Wewe ndio mwenye bongo fleva kaka. Nilipokua kidato cha nne nilibahatika kuhudhuria shoo zako mbili moja ilikua rais wa Marekani amekuja Bil clinton ikawa shoo ya wazi pale karibu na Pugu Sekondari na mimi nilkua mwanafunz wa Airwing na tulikuja kishule kumpokea ilikua mwaka 2006 kama sio 2004 na nyingne ni karibu na maskani Banana ukonga ilikua 2007 ilikua shiida kipind iko tuna copy na ku paste mashahiri yako tunajifanya na sisi Artist nakukubali sana na album zako mbili ya Nini chanzo
na Ugali mpka leo ninazo sema zimekaa tu maana ni tape na sasa tupo digital."

No comments:
Post a Comment