.

.

TUMIA VIDOLE

TUMIA VIDOLE
PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918 PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918sundwa.Blogspot.com

Tuesday, September 30, 2014

Ronaldo vs mess

Si jambo la ajabu kwa Kijana wa miaka ya 80 akikusimulia jinsi Diego Maradona alivyowaua England kwa bao lake la “Mkono Wa Mungu” katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1986. Bila Shaka Vijana wa kipindi hicho wanaweza kukupa mambo mengi yanayomhusu mkali huyu Maradona ambaye alikuja kumfunika Pele wa Brazil ambaye yeye naye alitamba vilivyo miaka ya 70. Hakuna Kijana Mpenda Soka wa wakati huo ambaye hakuwafahamu hawa Watu. Tofauti kubwa kati yao ilikua ni Pele alikua mzuri sana katika kufunga magoli Yani huyu alikua hatanii akionana na lango la timu pinzani yeye ni kufunga tu na inasemekana alifikisha magoli zaidi ya 1,000 katika maisha yake ya soka Lakini Diego Maradona yeye licha ya kufunga huyu jamaa alikua na kipaji kikubwa sana cha kuchezea mpira. Alikua ana uwezo wa kupiga Chenga kuanzia katikati ya Uwanja mpaka akafunga alikua anavutia mno kumtazama. Japokua Miaka imepita ila Hawa jamaa bado Dunia inawaheshimu mno kwa jinsi walivyolitendea haki Soka wataheshimika sana hawa watu kwa Wapenda Soka hasa Vijana wa miaka hiyo ya 70 na 80. Wakati Dunia inaonekana kutowasahau watu hawa Je Ulishajiuliza itakuaje Miaka 20 Ijayo? Je Ulimwengu wa Soka Utamkumbuka mchezaji gani wa kizazi hiki tulichonacho? Jibu ni rahisi mno CRISTIANO RONALDO na LIONEL MESSI. Yes!! nawazungumzia Cristiano Ronaldo Mchezaji wa Mabingwa wa Ulaya Real Madrid na nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno pamoja na mwenzake Lionel Messi mchezaji wa Barcelona na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Argentina. Hawa ni wachezaji wawili ambao kila kukicha wanavunja rekodi ambazo miaka mingi imepita watu wameshindwa Kuzivunja. Ni wachezaji ambao Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anadhani wanalingana kila kitu na hakuna ubishi katika hili. WANAFANA KILA KITU KASORO SURA Ronaldo na Messi wanafana katika vitu vingi sana na hapo ndipo Wapenda Soka wanaposhindwa kuwatofautisha. Yani ili umsifie Ronaldo inabidi Umwangalie Messi huu ni mfanano wa kimaendeleo kwao na unawafanya kila siku kuzidi kuishangaza dunia. Sababu kubwa inayofanya watu wapige kelele kila mwaka linapokuja swala la kumchagua mchezaji bora wa Dunia ni kwakua Uwezo wao unafanana. Hivi ulishawahi kujiuliza Ingekua Vipi kama Duniani angekuwepo Ronaldo peke yake au Messi peke yake katika viwango walivyonavyo? Hakuna Tuzo ambayo ungemnyima hapo na hapa ndo panapotupa utata linapofikia swala la kumchagua mchezaji bora wa Dunia. Baadhi ya ya vitu vinavyowafanya wafanane sana: Wote Wanacheza katika Ligi kuu Nchini Hispania (La liga) katika klabu kubwa za Nchi hiyo lakini pia wote ni Manahodha wa Timu zao za Taifa. Kila mmoja wao ana mtoto mmoja wa Kiume mtoto wa Ronaldo akiitwa Cristiano Ronaldo jr na yule wa Messi anaitwa Thiago. Tangu Ronaldo alipojiunga na Real Madrid mwaka 2009 Ameshafunga mabao 186 katika michezo 169 aliyoichezea Real Madrid katika Ligi kuu Hispania (La liga) Kwa Upande wa Messi yeye tangu Ronaldo alipofika katika Ardhi ya Hispania mwaka 2009 ameshafunga mabao 277 katika mechi 270 za Ligi kuu. Ronaldo ameshafunga mabao 53 katika mechi 52 za Michuano ya Ulaya Tangu alipojiunga na Real madrid wakati Messi amefunga magoli 59 katika mechi 63 alizoichezea Barcelona katika michuano ya Ulaya tangu Ronaldo alipofika Hispania. Messi ni mshindi mara 3 wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia maarufu kama Ballon d’or inayotolewa na FIFA na hii ni kuanzia mwaka 2009 tu wakati Ronaldo amepata Tuzo hii mara yake ya kwanza akiwa na Real Madrid. (Messi ana Jumla ya Tuzo hizo 4 na Ronaldo Jumla anazo 2 katika historia) BAADHI YA REKODI ZILIZOWEKWA NA WAKALI HAWA LIONEL MESSI Huyu ndiyo mshindi mara nne wa Tuzo ya Mchezaji bora wa FIFA wa Dunia Akishinda mwaka 2009,2010,2011 na 2012 ndo mtu wa kwanza kushinda Tuzo zote hizi katika ngazi ya mchezaji Messi ndo mchezaji ambaye jina lake limeingia katika orodha ya Mchezaji aliyefunga magoli mengi ndani ya mwaka mmoja akiwa amefunga magoli 91 mwaka 2012 hakuna mchezaji aliyewahi kufikia kiwango hicho. Messi ndo mchezaji aliyefunga katika mechi 21 mfululizo akiwa amefunga magoli 33 katika mara hizo 21. Messi ndie mchezaji wa kwanza kuzifunga timu zote katika ligi kubwa akifanya hivo katika Ligi kuu nchini Hispania. Ameshinda Tuzo ya Mfungaji bora wa Ligi kuu nchini Hispania maafufu kama Pichichi mara 3 yani mwaka 2010,2012,2013 Messi ndiye mchezaji wa Kwanza kuwahi kufunga magoli 200 katika Ligi kuu Nchini Hispania akiwa na umri mdogo (Miaka 25) Huyu ndiye mchezaji aliyefunga Hat Trick (Magoli matatu) nyingi katika mechi kubwa ya El Clasico (Barcelona vs Real Madrid) amefunga mara mbili. Messi amecheza Jumla ya mechi 550 katika maisha yake ya soka akifunga magoli 407 kati ya hayo 365 akifunga katika ngazi ya klabu na 42 akiwa ameifungia timu ya Taifa ya Argentina. CRISTIANO RONALDO Kabla ya mwaka 2013 huyu ndiye alikua Mchezaji ghali kabisa kuwahi kutokea katika Historia ya soka. Ndiye Mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 40 kwa msimu katika misimu miwili mfululizo . Ronaldo amecheza mechi 684 katika maisha yake ya Soka akiwa amefunga magoli 427 kati ya hayo 377 akifunga katika ngazi ya klabu huku 50 akiwa ameyafunga akiwa na Timu ya taifa ya Ureno. Mshindi mara mbili wa Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia wa FIFA akiitwaa mwaka 2008 na mwaka 2013. Ronaldo ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa Ligi kuu Spain (Pichichi) mara mbili yani msimu wa mwaka 2010/2011 na msimu wa 2013/2014 Ameshinda Tuzo ya Mchezaji bora wa msimu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2013/2014 Ndiye mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi katika msimu mmoja wa ligi ya Mabingwa Ulaya akifunga magoli 17 katika msimu wa 2013/2014 hii haijawahi kutokea. Ronaldo ndiye mchezaji pekee katika ligi ya mabingwa Ulaya aliyefunga magoli katika mechi 8 mfululizo katika msimu wa 2013/2014. Ndiye Mchezaji aliyefunga magoli mengi katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya akifunga magoli 9katika msimu mmoja. Ndiye mchezaji wa Kwanza La Liga kufunga magoli 150 katika ligi ikiwa ni kipindi kifupi kabisa kuwahi kutokea kwa mchezaji Hawa ni watu ambao wana uhakika wa kufunga goli zaidi ya 20 kila msimu. Ni wachezaji ambao wanacheza katika wakati huu ambao umetawaliwa na mabeki wenye Roho mbaya ambao ni ngumu kukuruhusu kuwapita lakini bado jamaa wanapita na wanafunga, wakati ambao timu nyingi zimetawaliwa na mifumo ya kupaki bus lakini bado jamaa wanafunga. Unataka nini katika Soka kama sio kuwaona hawa jamaa na kama hujampenda mmoja basi utampenda na kumkubali mwingine au uwakubali wote. Yapo mengi ya kuweza kusimulia baada ya miaka 20 ijayo kuwahusu wakali hawa Ronaldo na Messi.Ni Jambo la kuzidi kumwomba Mungu atupe miaka zaidi ya 20 ijayo ili tuwe na kitu kizuri kilichokamilika tunachoweza kuwahadithia watoto na wajukuu zetu. Pengine anaweza kutokea mtu mwingine atakayewafunika hawa lakini kwasasa HABARI ZOTE ZA SOKA ZIMETAWALIWA NAO.

No comments:

Post a Comment