Tuesday, September 30, 2014
Hatimaye crouch amvuruga padrew
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Liverpool ambaye sasa anakipiga kwenye timu ya Stoke City, Peter Crouch usiku wa jana aliifungia timu yake bao pekee kwa kichwa maridadi baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na victor Mosses dakika ya 15 ya mchezo.
Bao hilo limemuweka kwenye hali mbaya kocha wa Newcastle, Allan Pardew.
Newcastle united inayokamata nafasi ya 19 mpaka sasa haijashinda mchezo hata mmoja wa ligi kuu baada ya kutoa sare mechi tatu na kufungwa mechi 3 katika michezo 6 waliyocheza mpaka sasa .
Mashabiki wa Newcastle usiku wa jana waliingia uwanjani na mabango ya kumhamasisha bosi Mike Ashley amtimue kocha Pardew.
Huu ni mwanzo mbaya wa ligi kwa newcastle, mara ya mwisho kuanza ligi vibaya kama msimu huu ni miaka 11 iliyopita.......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment