.

.

TUMIA VIDOLE

TUMIA VIDOLE
PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918 PATA HABARI MBALI MBALI KUTOKA KATIKA BLOG HII PIA TANGAZA AU TOA MAONI KUPITIA Email:Luzunhowhiser@gmail.com OR Cell: 0653394330 OR 0755560918sundwa.Blogspot.com

Wednesday, July 15, 2015

HISTORIA MPYA MACHESTER UNITED

Bastian 9Bastian 10
Bastian Schweinsteiger ni miongoni mwa nyota wapya waliosajiliwa siku za hivi karibuni chini ya kocha mkuu wa kikosi cha Man United Louis van Gaal, mchezaji huyo amefurahi kuwa mchezaji wa kwanza wa Kijerumani kucheza kwenye klabu ya Manchester United huku akiamini ataweza kufanya kazi  nzuri msimu huu.

Mshindi huyo wa kombe la dunia mwaka 2014 alijiunga na ‘Mashetani Wekundu’ kwa dau la pauni milioni 15 akitokea Bayer Munich Jumamosi iliyopita na anategemewa kuleta mabadiliko kwenye nafasi ya kiungo kwenye timu ya United.

Bastian 10Schweinsteiger amefurahia kuwa mchezaji wa kwanza wa nchi yake kucheza Manchester United na ameiambia MUTV (Manchester United Television): “Ni heshima kubwa. Nilishataniana na Wayne Rooney kuhusu jambo hili kabla, lakini ni heshima kubwa kuwa Mjerumani wa kwanza kucheza hapa. Najisikia vizuri”amesema.

Akiwa amecheza miaka 17 kwenye kikosi cha Bayern Munich ndani ya Bundesliga, Schweinsteiger amefurahishwa na uhamisho wake wa kujiunga kwenye ligi kuu England (EPL) ambayo amekuwa akiifuatilia mara kwa mara.

Bastian 11“Nimekuwa nikiangalia sana mechi za ligi kuu ya England, kuna baadhi ya wachezaji wa kijerumani wanacheza Arsenal lakini Lukas Podolski ni rafikiangu na tulizungumza juu ya ligi hii”

“Kila mechi ni ngumu na inavutia, kwahiyo natazama mbele kukutana na mechi hizo kwa kiwango cha juu. Nafikiri tunatimu nzuri ambayo inaweza kufanya kazi nzuri”

Schweinsteiger ambaye atafikisha miaka 31 mwezi Agosti ameweka wazi kuwa, Louis van Gaal sio sababu pekee iliyomfanya ahamie Old Trafford.

Wakati kiungo huyo akifanya kazi na Van Gaal miaka miwili iliyopita kwenye kikosi cha Bayern, Schweinsteiger amesisitiza ukubwa wa klabu (Man United) ilikuwa ni sababu kubwa iliyomvuta na kuamua kufanya maamuzi ya kuhamia England.

“Ni kweli, namfahamu (Van Gaal) na ilikuwa rahisi. Sio kwasababu yake, japokuwa sababu kubwa imekuwa ni klabu, Manchester United”

“Ni klabu kubwa yenye utamaduni na ubora mkubwa  nafikiri tuna uwezo wa kushinda mataji msimu huu”

“Louis ni kocha mzuri na kilakitu ni kizuri, tutaona jinsi gani tutakavyofanya kwenye ligi”.

No comments:

Post a Comment