
Dili la Arsenal kumsajili nyota kutoka klabu ya Spoting Lisbon ya Ureno William Carvalho limeota mbawa baada ya kiungo huyo kuumia na atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki 10 hadi 12 sawa miezi mitatu.
Carvalho ambaye mara kwa mara amekuwa akihusishwa kusajiliwa na Arsenal atakuwa nje kwa miezi michache ijayo ya msimu unaokuja baada ya kuvunjika kwa mfupa unaoitwa ‘tibia’.
WilliamMchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa ni sehemu muhimu kwenye kikosi cha Ureno chini ya miaka 21 kwenye michuano ya European Championship ambapo alitajwa kama mchezaji bora wa mashindano baada ya kuonesha kiwango cha hali ya juu kwnye mechi dhidi ya Jamhuri ya Czech.
William 2Mwanzoni Manchester United walionesha nia ya kumtaka mchezaji huyo kabla ya kubadili mipango yao na kwenda kwa viungo Morgan Schneiderling na Bastian Schweinsteiger.
No comments:
Post a Comment