
WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu, huku wakihakikisha wanamchagua kiongozi atakayeweza kuzisimamia vizuri rasilimali za taifa kwa manufaa ya watu wote.
Kauli hiyo ilitolewa na Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya upadrisho kwa mapadri watatu wa jimbo hilo uliofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Watakatifu Mashahidi wa Uganda, Magomeni.
Askofu Mdoe alisema, kiongozi anayetakiwa kuchaguliwa na Watanzania ni yule mwenye hofu ya Mungu atakayewajali wananchi na kuwa na uchungu na rasilimali za taifa kwa maslahi ya watu wote na siyo mtu mmoja mmoja.
Aidha aliwataka kuwa macho na kuachana na ushabiki wa vyama kwani wakifanya hivyo wanaweza kuchagua mtu asiyestahili na asiye na sifa za kuongoza taifa.
“Sisi hatuna vyama, wananchi na wao wasifuate ushabiki wa vyama wachague mchamungu atakayeweza kuzisimamia rasilimali kwa maslahi ya taifa zima na hivyo ndivyo mungu anataka. Ninachowaambia watafute mtu makini,” alisema Askofu Mdoe.
Alisema katika kuelekea uchaguzi mkuu ndiyo kipindi ambacho watu wanahitaji kuongeza umakini wao ili kumchagua kiongozi. Akizungumzia upadrisho alioufanya kwa mashemasi waliopandishwa daraja la upadri alisema, jimbo la Dar es Salaam ni kubwa hivyo linahitaji wachungaji wengi watakaowaongoza waumini wa jimbo hilo
No comments:
Post a Comment