SIKU moja tu baada ya Tume ya Uchaguzi (ZEC) kutangaza mipaka ya
majimbo mapya ya uchaguzi, baadhi ya viongozi wametangaza nia ya kuwania
nafasi za Uwakilishi na Ubunge katika majimbo hayo.
Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi ametangaza kuwania Uwakilishi katika jimbo jipya la Mahonda kutokana na jimbo lake la Kitope kufutwa katika mabadiliko mapya ya majimbo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi.
Aidha, pia alitumia nafasi hiyo kuaga watendaji na viongozi wenzake kwa ushirikiano makubwa kutokana na mabadiliko ya jimbo hilo pamoja na shehia zake.
Akizungumza na viongozi wa kamati ya siasa na ya utekelezaji ya jimbo, balozi alipongeza wananchi na viongozi hao kwa juhudi kubwa za kusimamia maendeleo.
Alisema, wakati akiwa Mbunge wa jimbo la Kitope, alikuta likiwa na miundombinu mibovu ikiwemo ya maji safi na salama, umeme pamoja na shule na hospitali.
“Viongozi wenzangu wa kamati ya siasa na halmashauri kuu nachukuwa nafasi hii kuwaaga na kuwapongezeni kwa mashirikiano yenu ambayo yamefanikisha na kulifanya jimbo la Kitopewa kuwa la mfano wa kuigwa,”alisema.
Mbunge wa Viti Maalumu, kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja, Kidawa Hamid Saleh ametangaza nia ya kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo jipya la uchaguzi la Mahonda.
Kidawa, ambaye ni mchumi na mwanzilishi wa mfuko wa kujitegemea wenye lengo la kuwawezesha wajasiriamali kupiga hatua kubwa ya maendeleo, alisema atagombea jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.
Alisema amepata uzoefu wa kutosha kutoka katika viti maalumu na sasa ameamua kuwachia wenzake kugombea nafasi hizo. “Nimepata uzoefu wa kutosha wakati nikiwa mbunge wa viti maalumu na sasa nipo tayari kugombea jimbo la Mahonda na nafasi ya viti maalumu nawaachia wanachama wenzangu,” alisema Kidawa.
Kidawa aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Oganaizesheni wa CCM Taifa na sasa ni Mwenyekiti wa Bunge. Pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati huduma za jamii katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mchuano mkali zaidi unatazamiwa kujitokeza katika kuwania majimbo mapya yaliyopo katika mkoa wa mjini magharibi Unguja ikiwemo jimbo la Pangawe, Kijitoupele, Mto Pepo na Welezo ambapo tayari baadhi ya wanachama wa CCM wameanza kujipanga.
Taarifa zaidi zinazoonesha kwamba baadhi ya watendaji waliopo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo makatibu wakuu na wakurugenzi wa taasisi mbali mbali wapo katika hatua za mwisho kujitoza katika kinyang’anyiro cha nafasi za uongozi wa Ubunge na Uwakilishi.
Kwa mujibu wa masharti ya utumishi ya Serikalini ya Mapinduzi ya Zanzibar, watumishi wa Serikali wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi, watalazimika kwanza kuandika barua na kuchukuwa likizo bila yamalipo.

No comments:
Post a Comment