MICHEZO: Kimataifa
Barcelona jana usiku imeichapa 3-0 AS Roma katika mechi ya kirafiki iliyopigwa uwanja wa Nou Camp, mjini Barcelona, Hispania.
CHANZO: shafii Dauda
Barcelona jana usiku imeichapa 3-0 AS Roma katika mechi ya kirafiki iliyopigwa uwanja wa Nou Camp, mjini Barcelona, Hispania.
Magoli ya Barca yalifungwa na Neymar (27), Lionel Messi (41) na Ivan Rakitic (66).
Moja ya tukio lililovuta hisia za mashabiki wengi ni pale ambapo Messi alinusurika kupata kadi nyekundu kufuatia kumpiga kichwa Mapou Yanga-Mbiwa.
Mfaransa, Mapou alikwaruzana na Messi ambapo akamuwekea kichwa Messi ambaye alijibu mapigo kwa kumgonga ‘bichwa’, lakini refa akampotezea Supastaa huyo na kuwaonyesha wote wawili kadi ya njano.
Refa huyo Mhispania, Javier Estrada Fernandez alitakiwa kumuonyesha kadi nyekundu Mapou kwa kitendo cha kumpiga kichwa Messi, lakini naye ilistahili kadi nyekundu kwa kujibu mapigo.
CHANZO: shafii Dauda
No comments:
Post a Comment