Cheki mfululizo wa Majeruhi kwa Wilshere.
MICHEZO:
Hizi ni taarifa mbaya kwa mashabiki wa Arsenal wakati huu timu yao inaelekea kuanza msimu mpya wa ligi kuu England ikiwa na matumaini ya kuipindua Chelsea.
Arsenal chini ya Arsene Wenger wanaamini sasa umefika wakati wa kuchukua ubingwa ambao upo mikononi mwa Jose Mourinho.
Hata hivyo, hofu imetanda Emirates baada ya vipimo kuonesha kwamba Jack Wilshere anaweza kukaa nje ya uwanja wa muda mrefu baada ya kuonekana kuna jeraha kubwa katika kifundo chake cha mguu alichoumia.
Arsenal wanatarajia kufanya uchunguzi zaidi mwishoni mwa juma hili, lakini hali inavyoonesha Wilshere anaweza kukaa nje ya uwanja kwa wiki sita hadi nane.
CHANZO:shafii Dauda
No comments:
Post a Comment