HABARI ZA KIMATAIFA:
Naye musuluhishi wa zamani kunako mugogoro wa Burundi bwana Abdoulah Bartele amesema kwamba kazi yake imefikia kikomo pale walipo wakabizi jukumu ya usuluhisi ma raisi wa jumuhia ya Afrika Mashariki, ambao pia amelaumu kwakutochukuwa hatua sahihi kutokana na hali ya sasa nchini Burundi. Ameonesha masikitiko yake cha maraisi wa umoja Mashariki, alikuwa musuluishi wa mugogoro wa Burundi ametoa maoni yake kutoka na kikao cha maraisi wa Afrika mashariki, amestahajabishwa na matokeo ya mukutano uwo ambapo serekali ya Nkurunziza imeombwa kuharirishwa chaguzi za raisi za tarere 15 julai kwenda tarehe 30 Julai, ili musuluhishi mpya wa kanda la umoja wa Afrika mashariki, mweshimiwa Kaguta Yoweri Museveni awe amekwisha sikiliza pande zote yaani serikali ya Nkurunziza na vyama vipinzani pia makundi yote aramu zinazo bebelea silaha ziweze kunyanganywa ikiwemo kundi Imbonera Kure tawi ya vizana ya chama tawala CNDD-FDD . Bwana Bartele anakubali kwamba usuluhishi kwasasa umeachiwa kanda la Afrika Mashariki na kwamba kwa hisia zake na utahalam wake, mnamo siku 15 aiwezekani kuweka hali ya uchaguzi bora na yenye mwnga nchini Burundi, kwani swala tete la ungombeaji wa muula wa tatu wa Raisi Nkurunziza aukuzungumuzwa kwenye kikao cha maraisi wa Afrika mashariki. Ameendelea na kusema kwamba umoja wa mataifa aujautupilia mbali nchi ya Burundi. Ameendelea na kuonesha nchini Burundi hali ya salama sio nzuri kama wanavyo dai viongozi kutoka chama tawala CNDD-FDD. Ametowa mfano fupi mwenye kiti wa bunge muheshimiwa Pi Navyohanyuma na makamu wa pili wa raisi Muheshimiwa bwana Gervais Rufikiri, wametoka nchini na kujielekeza Ubeljiji kwa jkuofia usalama wao, amemalizia na kusema hali hii inaonesha ni gisi gani muzozo ni mkubwa mno na unaweza kuathiri nchi jirani iwapo aitapatiwa ufumbuzi maridhawa. Tuwafaamishe kuwa nchi ya Burundi imepoteza sifa kemkem ambazo ilikua inajikusanyia miaka iliopita kunako idara mbalimbali.
No comments:
Post a Comment