Pichan ni muaninia kiti cha uraisi kupita chama cha ccm,Dr john magufuli
Chama Cha Mapinduzi(CCM), mkoa wa Dar es Salaam, kinatarajia kumtambulisha kwa wananchi, mgombea urais wake, Dk. John Magufuli na mgombea mwenza wake, Samia Hassan Suluhu, leo kwenye viwanja vya Mbagala Zakhiem.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba, aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa mkutano huo utaanza majira ya mchana.
“CCM sasa hatuna shaka na ushindi wetu, mgombea tuliyenaye ni mchapa kazi, Watanzania na wana-CCM tunamuamni,” alisema Simba.
Kuhusu makundi ndani ya chama, alisema sasa wamekuwa kitu kimoja na kwamba wote ni kundi la CCM, baada ya mchakato wa kutangaza nia kumalizika na hivyo mgombea huyo ataungwa mkono.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholaus Mgaya, alisema anaamini mgombea huyo aliyeteuliwa na CCM, ataongoza vyema vita dhidi ya rushwa na wizi wa mali za umma.
Akizungumza kwa niaba ya Tucta jana, alisema wana imani na utendaji wa Dk. Magufuli, hivyo wanatarajia kupambana na matumizi mabaya ya madaraka kwa kuonea wanyonge na kurekebisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na matatizo ya wafanyakazi.
“Kwa niaba ya Tucta, tunaipongeza CCM kuanzia mchakato mzima ulivyoanza na namna walivyopata mgombea wake, tuna imani akipata nafasi hiyo wataongeza kasi ya kupambana na haya niliyoyaeleza hasa rushwa na wizi wa fedha na mali za umma,” alisema Mgaya.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment