Tuesday, September 30, 2014
KWETU KWA ZULU
BAADA ya kuzamia Ulaya, jamaa yetu mmoja hatimaye akawa anaishi Uswisi. Lakini maisha yake yalikuwa ya kujifichaficha maana alikuwa hana vibali vya kuishi huko. Washikaji wenzie wakamwambia dawa hapa ni kufanya juu chini aoe mwanamke wa Kiswisi, hapo lazima atapata uraia.
Katika sakasaka hatimaye mama mmoja mzeemzee akaingia mkenge na kudhania anapendwa akakubali kuolewa na Mbongo. Mbongo akawa amejitambulisha kuwa eti yeye Mzulu anatoka Afrika ya Kusini, si unajua Wabongo wengine.
Ndoa ikafanyika mtoto wa Kizungu kajua kaolewa na Mzulu, kumbe mtoto wa Tandale.
Siku moja mama wa Kizungu karudi kwa mumewe akiwa na furaha sana, “mume wangu leo nimekutana na Mswisi mwenzangu naye kaolewa na bwana Mzulu kama wewe, nimewakaribisha Jumapili waje kwa chakula cha mchana ili mkumbushane mambo ya kwenu.”
Jamaa yetu mkojo ulimbana ghafla, akajua kuwa sasa mambo ndiyo yameharibika, alikuwa anaiona laivu safari ya kurudishwa Bongo kwa kosa la utapeli.
Usiku wa Jumamosi alikesha mimacho imemtoka akawa anajaribu kukumbuka hata neno moja la Kizulu alilowahi kusikia, hakukumbuka, miji ya Sauzi aliyoikumbuka ilikuwa Soweto na Johannesburg, na pia akakumbuka Kwa Zulu Natal, akaona jamaa akifika atang’ang’ania kuwa katoka Kwa Zulu Natal, basi mengine atajifanya bubu.
Jumapili ikaingia siku yake ya kuumbuka ikawa imefika.
Hatimaye wageni wakaingia, kina mama wa kizungu wakawa katika furaha za kuwa na waume waafrika tena wote Wazulu. Akina mama wakasema wao wanaenda jikoni ili jamaa waongee kikwao.
Jamaa yangu akawa anamuangalia mwenzake kichwani anajiuliza huyu Mzulu namuanzaje ili asiharibu mambo? Si akaanza kujisema kwa nguvu, “Sasa huu msala huu mi Kizulu nakijulia wapi?” Hee ghafla yule mgeni akarukia, “Aise unajua Kiswahili?”
“Ndugu yangu kwa nini nisijue Kiswahili? Nihifadhi ndugu yangu mi natoka Tanzania, nimezaliwa Tandale huyu demu nimemdanganya mi Mzulu”.
Mgeni naye akajibu, “Aise Mungu ashukuriwe na mimi nilidhani we Mzulu, maana miye natoka Mbeya nilimdanganya huyu wangu kuwa natoka Sauzi, hapa nilikuwa sina raha najua we Mzulu, na huyu mama akijua nilikuwa namdanganya atanishtaki na safari ya kurudi Bongo itakamilika. Hebu tuwaite tuwaambie kumbe tunatoka kijiji kimoja nje kidogo ya Kwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment