
Profesa Jay, ambaye alikuwa akisaidiana na msanii mwenzake Mbunge wa Mbyea Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, walikuwa wakitambulisha nyimbo yao inayokwenda kwa jina la M4C, ambayo wataiimbia katika ziara iliyopewa jina la M4C Tour itakayoanza hivi karibuni.
Viongozi, wanachama na waalikwa wengine, walianza kushangilia mara tu mshehereshaji wa uzinduzi wa CHADEMA Mtandao, Ester Wasira alipowataka Profesa Jay na Sugu wapande jukwaani kutumbuiza kidogo na kuelezea namna watakavyofanya ziara yao ya nchi nzima.
Kelele za kushangilia na kuonyesha vidole vitatu zilisikika wakati wasanii hao wakichana mistari
No comments:
Post a Comment