“Ujanja mwingi mwisho giza” walishawahi kusema wahenga. Huu ulaghai wa ndugu zangu wahafidhina kamwe hauwezi kututoa katika mstari na hii misamiati ya kutulainisha ya MAFUTA NA GESI, haitusaidii.
Inasikitisha kuwa viongozi wetu wanawafanyia hadaa wazanzibari kwa kuwapaka mafuta. Viongozi tuliotegemea wawe imara na wakweli wa nafsi zao leo wameamua kuwa wapiga zumari na wanatumbuiza kwa nyimbo za mafuta eti watu wawakubali na kuuwa AJENDA yao. Agenda ya Zanzibar. haikubaliki.
Baada ya kufanya kila ghilba na hadaa na mazingaiombwe ya katiba. Viongozi hawa wanajifanya hawajui kuwa ule mchakato kule BUNGENI haukukidhi matakwa na ulilazimishwa, Badala ya kutuambia UHALALI wa katiba iliyopendekezwa ukoje, wamerukia MAFUTA NA GESI. Kilemba cha Ukoka.
Badala ya kutuambia Vipi mshirika wa muungano ameibuliwa na kuwekwa wazi ili tuwe na muungano imara wa heshima, wanatuletea hadithi ya Zanzibar eti kukubaliwa kukopa.Ina maana kilio cha wazanzibari katika muungano huu ilikuwa ni kutaka kuruhusiwa kukopa na wala si MFUMO mzuri wenye kutoa haki kwa kila mshirika? yaani kwamba sisi Zanzibar nafasi yetu katika muungano iwe ni kuomba ridhaa kwa mshirika aliyejiguza kuwa ndiye muungano wenyewe? Mbona masuali haya hamtujibu?
Badala ya kutuambia vipi Katiba hii haitaathiri katiba ya Zanzibar na MAMLAKA YA ZANZIBAR mnakuja na habari ya rais kuwa makamo wa pili lakini hawajatwambia atakuwa na athari gani ya kiutendaji. Wamesahau kuwa bado tatizo liko pale pale hata akiwa hivyo huyu ni makamo wa serikali ya jamuhuri ambayo bado ni Tanganyika .
Wameshindwa kutwambia vipi masuala ambayo si ya muungano kwa Tanganyika yatajitenga na kusimamiwa na serikali ya jamuhuri na kufaidi huduma za serikali ya jamuhuri wakati kiukweli ni ya Tanganyika halafu wanatwambia tuyakubali haya. kwani hivi sasa tunapopiga kelele kwa haya si mfumo ndio uko hivo? lipi jipya hapa.
Wameshindwa kutwambia vipi ule ‘UKUU WA SHERIA WA KATIBA hii iliyopendekkezwa” uataepuka kuinyanganya nguvu katiba ya Zanzibar?
na wanakuja ya hadithi ya Wapinzani kutoitakia mema Zanzibar, kisa walitoka na hawakuwa tayari kuidalali Zanzibar kama walivyofanya wao.
na wanakuja ya hadithi ya Wapinzani kutoitakia mema Zanzibar, kisa walitoka na hawakuwa tayari kuidalali Zanzibar kama walivyofanya wao.
Wameshindwa kutwambia vipi vile vyanzo vya mapato vya jamuhuri ya Muungano vinainyima vipi nguvu ya uchumi wa Zanzibar na wamekuja na habari ya wafanyakazi wa Muungano walioko Zanzibar kuchangia mafao yao Zanzibar halafu iweje?
Baada ya yote hayo wanatuhadaa tuikubali na eti wanatushawishi tuwaunge mkono kwa lipi? yaani tukubali kufuta mamlaka yetu mbali mbali tuliyopewa na katiba yetu na tukubali kujitawealisha kwa mshirika mwezetu?
Binafsi nilitarajia aje waziri wetu wa fedha atufafanulie vipi tunaweza kuwa huru kiuchumi na kujitegemea kwa maendeleo yetu, kufafanua vyanzo vyetu vya mapato na uwezo wa kukusanya leo anakuja mkuya na Hadidthi ya kukopa tena hadi idhini na dhamana itolewe na Mshirika.
NIWAKUMBUSHE.
Hicho sio kilio tena na kamwe hayo mliyoyasema sio hoja za kilio cha kutaka katiba mpya. Hapa TATIZO NI MFUMO badala ya kuhangaika kutengeneza mfumo imara utakaohakikisha haki za kila mshirika mnatuletea CHUPA YA MAFUTA NA GESI? mnaleta kivuli cha makamo wa rais wa pili wa muungano wa karatasi asiye na meno, kibogoyo na makamo wa kuchora ?
Niwakumbushe kuwa Zanzibar ni NCHI na rais wake kapewa nguvu za kikatiba kugawa Zanzibar kadiri anavyoona inafaa na hakushurutishwa kushauriyana na yoyote. Kwani hivi sasa huyo rais Wa SMT hayupo? mbona hakuambiwa ashauriane naye? hili hamlioni?
Niwakumbushe kuwa Katiba ya Zanzibar imewapa Mamlaka wananchi kuamua mustkbali wao kwa mambo yote makubwa na muhimu leo mnataka kunyanganya malaka hayo na mnataka wasaini kwa mikono yao yao kujinyanganyanya nguvu hio?
BADO KABISA na Agenda ya Zanzibar iko pale pale na kamwe haitakufa kwa kupakwa MAFUTA NA GESI .
Tuungane kuitetea Zanzibar
No comments:
Post a Comment